Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange aahidi kushirikiana na Tarura na Dawasa kufuatilia miradi ambayo haijakamilika, kukamilika ili wananchi waweze kupata huduma zote za kijamii.
“Mm pamoja na Madiwani tunarajia kuanza ziara kutembelea mitaa mbalimbali ili kuangalia miradi ambayo haijamilika kuifatilia na kutoa elimu kwa jamii namna ya kulinda miradi iliyokamilika,”amesema
Hayo yamezungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na madiwani 19 wa kata mbalimbali.
Sambasamba na hayo amesema kuwa ataendelea kushirikiana na watendaji wote ikiwemo Madiwani na watumishi wote wa umma pamoja na Taasisi mbalimbali za kimaendeleo.

0 Comments