Na Nancy Mawole
KAMATI ya Ushauri Wilaya ya Ubungo(DCC)imejadili rasimu ya Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti na Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange ameongoza kikao hicho. Kikao hicho kimejadili mapendekezo ya mpango wa Bajeti Halmshauri yenye makisikio ya 143bn/-.
“ Kikao hichi kinaangazia zaidi kupata ushauri kutoka kwa wajumbe ikiwa lengo la mapendekezo ya bajeti ni kutelekeza miradi yenye kuleta tija katika jamii,” alisema
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibamba (CCM)Issa Mtemvu amesema Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya Manispaa yanalenga kwenye Maeneo mbalimbali kama vile vituo vya afya, shule, Zahanati na miradi mingine.
Aliongezea na kusema kuwa mapendekezo hayo yamehusisha pia kuendeleza sekta ya michezo.
Kikao hicho kilihusisha wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya siasa. Wajumbe hao walipata wasaa wa kuwasilisha hoja zao ili kufanya maboresho ya mpango wa Bajeti hiyo kwa maslahi mapana ya jamii.


0 Comments