TANZANIA KULITANGAZA SOKO LA KARIAKOO KIMATAIFA









MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kwa kushirikiana na Jumuiya ya wafanyabiashara kuandaa safari maalumu ya kulitangaza soko la kariakoo wazi masaa 24 kwenye nchi jirani ikiwemo Lusaka,Zambia, Lilongwe Malawi, congo, Rwanda na Burundi


Ameyasema hayo wakati wa uzunduzi wa ufanyaji biashara wa saa 24  uliofanyika katika soko la karikoo


Amesema wafanyabiashara 10 pesa zao za nauli zinatoka ofisi ya mkuu wa mkoa waende wakainadi nchi ya Dkt Samia Suluhu Hassan.


“Lengo la ziara hiyo ni kuonesha mafanikio anayoyafaa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwenyw nchi jirani pamoja na kuongeza uwekezaji nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi,”alisema 


Ametoa maelekezo kwa wasaidizi wake wiki ijayo ataunda kamati ya kupitia upya sheria ndogo ndogo za halmashauri zinazokinzana na wafanyabiashara wa saa 24 pamoja na kumshauri waziri wa tamisemi ili kuona namna tunavyoweza  kuziondoa na kuruhusu watu wafanye biashara masaa 24.


Alisema kuwa soko zitafungwa taa nyingi pamoja na kamera 40, zoezi hilo na pia amewahakikishia wafanyabiashara pamoja na wananchi ulinzi wa kutosha wakati wa kufanya biashara nyakati za usiku.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila amesema amesema katika kuboresha miundombinu ya umeme shirika la umeme la Tanzania limeanza kubadilisha nguzo za umeme kutoka za miti kwenda za zege katika eneo la kariakoo, pamoja na kubadilisha nyaya za wazi na kuweka zilizofunikwa hadi sasa kazi ya kubadilisha nguzo imekamilika kwa asilimia 90 na za kubadilisha nyaya imekamilika kwa asilimia 95.


Maeneo mengine yatakayofungua biashara saa 24 ni pamoja na Mwenge, Manzese, Tandika, Mbagala,Ubungo na Magufuli bus stand.

Post a Comment

0 Comments