VIJANA KUNUFAIKA KUPITIA KAMPUNI YA THE DIPLOMATS


KAMPUNI ya ‘The diplomats’ inatarajia kuajiri vijana wengi zaidi wenye taaluma na ujuzi wa kufuata itifaki kwa lengo la kuandaa matukio mbalimbali ya Kimataifa.


Kampuni hiyo inatoa huduma mbalimbali kwa bei nafuu ikiwemo kuandaa vifaa vinavyohitajika katika shughuli husika ‘bodyguards’, ‘ushers’.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni Anthony William jijini Dar es Salaam.


“ Sisi kampuni lengo ni kuwapatia vijana wa kitanzania ajira ambayo itawakwamua kiuchumi,”alisema 


Sambasamba na hayo ameahdi William amesema kampuni inatoa pia mafunzo kwa wale waliopo kwenye ajira na hawana ujuzi katika kazi zao.


Amewakaribisha wadau mbali mbali kama vile Serikali, Benki, Sekta Binafsi na amesema kuwa kampuni ina vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.


Kwa upande wake Mdau wa Kampuni hiyo Anthony Luvanda amesema yeye ni mzoefu wa miaka 15 hivyo jambo la kuja wazo hili italeta watu wenye uzoefu katika masuala ya kiitifaki.


“ Kuna baadhi ya watu ambao hupewa ajira hizo lakini hawafati misingi ya taaluma ambayo imepelekea kupata ajira aliyo nayo. Hivyo basi kampuni itaajiri wenye ujuzi, heshima, maadili pamoja na lugha nzuri kwa wageni waalikwa katika shughuli husika,” alisema




Post a Comment

0 Comments