HALMASHAURI KUU YA CCM KIBAHA MJI YARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDELEO YA KIBAHA TC





VICTOR MASANGU, KIBAHA


Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha  kwa pamoja imeridhishwa na miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo maji, elimu, afya miundombinu ya barabarara pamoja na hudumu  nyingine za maendeleo iliyotekelzwa kwa kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi Disemba mwaka 2024.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu cha Utekelezaji wa Ilani ya CCM  kwa kipindi cha Julai 2024  hadi Desemba 2024 kilichohudhuria na viongozi wa chama pamoja na serikali kwa ajili  namna ya ilani ya chama ilivyotelekezwa katika miradi ya mbali mbali ya  maendeleo.


Nyamka amesema kwamba wameweza kupita katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ambapo kwa  kauli moja yameipitisha kutokana na kuona kazi nzuri ambayo yameifanya katika utekelezaji huo wa miradi ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa katika kuwasaidia  kwa kiais kikubwa wananchi kuweza  kupata huduma kwa urahisi katika mahitaji mbali mbali.


Aidha Nyamka amebaisha kwamba katika kikao hicho  wamewez kumpongeza  kwa dhati Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John kwa kuweza kupambana na kuweza  kusimamia kwa vitendo  utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwani miradi mbali mbali imeweza kutekelezwa.


Aidha kikao hicho kimempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya Kibaha mjini Dkt. Rogers Shemwelekwa  kwa kuwekakuweka mikakati mizuri ambayo imeweza kuongeza chachu zaidi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwemo sambamba na kusimamia maslahi ya watumishi wake.


Pia Mwenyekiti huyo hakusita kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe:Silvestry Koka  kwa kutekeleza majukumu yaoke ipasavyo ya kuwatumikia wananchi ikiwemo suala zima la kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo hali amabayo imechangia kwa kiais kikubwa kuweza kuleta chachu ya maendeleo.


Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba ameweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwani miradi mingi katika sekta mbali mbali ya maji, afya, elimu, miundombinu ya barabara pamoja na mambo mengine ya huduma za kijamii imeweza kutekelezeka  kwa kiwango kikubwa.


Kwa upande wake Katibu wa chama caha mapinduzi (CCM) Issack Kaleiya amesema kwamba miradi hiyo amabyo walipita kwa ajili ya kukagua ni moja ya utekeelzaji wa ilani ya chama na kwamba itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kutatua kero na changamoto  mbali mbali za  wananchi.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amebainisha kwamba katika Halmashauri ya Kibaha mji Ilani ya chama imeweza kutekelezwa katika miradi mbali mbali ya maendeleoa na kumshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Sauluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha ambazo zimekwenda kutekeleza miradi  ya maendeleo.

                                         

Post a Comment

0 Comments