RC PWANI AUNGURUMA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA URAIA NA UTAWALA BORA



NA VICTOR MASANGU,PWANI 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka watendaji wa Kata pamoja na wakuu wa usalaam wa Wilaya zote ndani ya Mkoa huo kuongeza juhudi za utendaji kazi hasa kwa kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao  kwani kufanya hivyo ni kutekeleza agizo la Rais wa nchi ambae amekuwa kisisitiza kuwa kipaumbele chake ni kuondoa kero kwa jamii


Kunenge ameyasema hayo  leo Jumatatu Machi 10,2025 wakati wa  mafunzo  ya uraia na utawala bora yaliyofanyika Mjini Kibaha chini ya   Wizara ya katiba na sheria  lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watumishi hao juu ya kuimarisha utendaji kazi wao


"Sisi sote tunamwakilisha mheshimiwa Rais wetu na kipaumbele chake ni kuondoa kero kwa wananchi wake hivyo tusipotekelza majukumu yetu sawsawa tutakuwa tuna muangusha jambo ambalo halitakiwi"amesema


Amewataka watendaji hao kuyatumia mafunzo hayo kwa kuboresha utendaji wao  na kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao jambo litakaloleta faida kulingana an malengo ya serikali 


"Mkiyatumia vizuri mafunzo haya italeta maana lakini kama mtayapuuza itakuwa hasara kwa muda uliotumika na hata gharama zilizotumika hivyo ni vema mkayafanyie kazi ili yalete tija" amesema.


Kwa upande wake  Mrakibu msaidizi wa Polisi Nicolaus Mhagama amewataka watendaji wa kata kuzingatia kanuni na sheria zilizopo pindi wanapowahudumia waannchi ili kuepusha migogoro isiyokuwa na ulazima


"Sasa hivi serikali imewaongezea nguvu kwa kuwaletea Polisi Kata hao ni watu muhimu ambao mnaweza kushirikiana nao huko kwa kuimarisha usalama" amesema


Mratibu wa mafunzo hayo  kutoka wizara ya katiba na sheria  wakili Prosper  Kisinini amesema kuwa serikali imeona umuhimu wa kuwapa mafunzo hayo watendaji wa ngazi mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii.




Post a Comment

0 Comments