VIJANA WAHIMIZWA KUWA MABALOZI WA MAZINGIRA




Na Nancy Mawole

SERIKALI imehimiza vijana ikiwemo wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa utunzaji mazingira kwa kupanda miti mingi mashuleni.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti wakati akizindua kampeni ya ‘Ishi kijanja Ishi Kijani’ shule ya Jokate Mwegelo mkoani Pwani. Kampeni hiyo imeasisiwa na WWF.

Sambasamba amewashukuru ( WWF)ilidhamini majiko mawili ya nishati safi ya kupikia yenye ujazo wa lita 200 . Lengo ni kufikia 2034 asilimia 80 wanatumja nishati safi ya kupikia.

“ Tunawashukuru wadau wetu muhimu kwa sappoti juhudi Serikali kupitia Raisi Dkt Samia ya kupanda miti kwa ajili ya kulinda mazingira ya nchi kwa vizazi vijavyo. Vilevile kuunga mkono campaign ya nishati safi inayolenga kila mtanzani kuepukana na nishati chafu,”alisema

Ikiwa juhudi ya serikali  ni kuiendeleza sekta ya elimu, Magoti aliwatambulisha waalimu wawili mmoja wa sayansi na mwingine wa biasahara.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa WFF Yohana Mpagama amesema kuwa ni miaka 3 sasa wanashirikiana na shule hiyo katika upandaji miti.

Ameongeza kuwa wataendelea kushirikiana na shule hiyo kwenye campaign ya utunzaji wa mazingira pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchi. 

Hata hivyo wanafunzi wa shule walipatiwa zawadi na serikali kutokana na ufaulu mzuri . Zawadi hizo ni mchele Kilo 100, Creti za soda, Tambi, Viazi. Hii ni motisha ya wanafunzi hawa kusoma huku wakipata mahitaji yao muhimu shuleni.

Post a Comment

0 Comments