Mc Garab Atangazwa Rasmi Kuwa Balozi wa SKYFARNET

 




Dar es Salaam – Kampuni ya SKYFARNET, mtoa huduma kinara wa Wireless Unlimited Internet nchini, imemtangaza rasmi GARA SUPER MAN – MC GARA B kuwa BALOZI WA SKYFARNET kuanzia leo. Uteuzi huu umetolewa kufuatia mchango mkubwa wa Mc Garab katika kuhamasisha matumizi ya huduma za SKYFARNET pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu kama mtumiaji wa huduma hizo nyumbani na ofisini.


Mc Garab amekuwa shabiki na mtetezi mkubwa wa huduma za SKYFARNET kutokana na kasi, uthabiti na ubora wake unaolingana na kiwango cha fiber, licha ya kuwa wireless. Uhalisia wa matumizi yake na uaminifu aliouonyesha kwa muda mrefu umemfanya kuwa chaguo sahihi la kuisemea kampuni hii mbele ya jamii.


Kwa kutangazwa kuwa balozi, Mc Garab sasa atashiriki kikamilifu katika:


Kueneza taarifa za vifurushi na kampeni za SKYFARNET


Kuhamasisha wananchi kujiunga na mtandao wa SKYFARNET


Kuitangaza huduma ya MCHONGO UNLIMITED – 10 MBPS


Kushiriki matukio, matamasha na kampeni zote za kampuni



SKYFARNET inaamini kuwa ushirikiano huu na Mc Garab utaleta nguvu mpya katika kufikisha huduma bora za intaneti kwa Watanzania wengi zaidi, hasa katika maeneo ambayo fiber haijafika.



---

Post a Comment

0 Comments