SKYFAR INTERNET YAZINDUA KAMPENI KUBWA YA “MCHONGO UNLIMITED” YENYE KIFURUSHI CHA 10 MBPS KWA TSH 65,000 TU

 




Leo Tarehe 26 December jijini Dar es salam 

Kampuni ya SKYFAR INTERNET leo imezindua kampeni yake kubwa ya mwaka ijulikanayo kama “MCHONGO UNLIMITED”, ikiwa ni juhudi za kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora na nafuu ya intaneti isiyo na kikomo jijini Dar es Salaam.


Kupitia kampeni hii, SKYFAR imeanzisha kifurushi kipya cha intaneti cha 10 MBPS kinachopatikana kwa Tsh 65,000 tu kwa mwezi, bila kikomo cha spidi. Kifurushi hiki kimebuniwa kuendana na mahitaji ya watumiaji wa nyumbani na ofisini, hususan katika msimu huu wa sikukuu ambapo hitaji la intaneti ya uhakika huongezeka kwa ajili ya kazi, burudani, mawasiliano na shughuli za kifamilia.


Aidha, wateja wote wanaojiunga kwa kulipia Tsh 65,000 watapata Free Installation pamoja na Free Router, ikiwa ni sehemu ya ofa maalum ya kampeni hiyo.


Kasi ya 10 MBPS inatosha kwa matumizi ya kawaida ya intaneti kama vile kuvinjari mitandao, kutazama video, mikutano ya mtandaoni, na matumizi mengine ya msingi ya kidijitali. Hata hivyo, SKYFAR inaeleza kuwa mahitaji maalum kama michezo ya mtandaoni au kutazama video za 4K yanaweza kuhitaji kasi za juu zaidi kulingana na matumizi ya mtumiaji.


SKYFAR INTERNET inaendelea kujitanua katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ikiendeleza dhamira yake ya kufanya Wireless Unlimited Internet kupatikana kwa urahisi hata katika maeneo ambayo huduma ya fiber bado haijafika.

Post a Comment

0 Comments