CHARLES MAKONGORO NYERERE ASHINDA SAFARI YA KWENDA CANADA KUPITIA KAMPENI YA CRDB TEMBO CARD




Mteja wa CRDB Bank, Charles Makongoro Nyerere, ameibuka mshindi wa safari ya kwenda nchini Canada kushuhudia mashindano ya FIFA World Cup kupitia kampeni ya matumizi ya Tembo Card inayoratibiwa na benki hiyo.

Charles ametangazwa mshindi katika droo maalum iliyofanyika leo, ambapo CRDB imeendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaotumia huduma za malipo ya kidigitali kupitia Tembo Card.




Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Charles amesema alianza kuitambua CRDB tangu kipindi benki hiyo ilipofungua huduma katika maeneo ya vijijini, jambo lililowafanya wananchi wengi kupata urahisi wa huduma za kifedha.

“Kwa mara ya kwanza niliwafahamu nilipokuwa kijijini baada ya CRDB kufungua tawi. Zamani matumizi ya card hayakuwa makubwa lakini sasa watu wengi wanafurahia kutumia CRDB Kiganjani,” amesema Charles.

Aidha, amewapongeza viongozi wa CRDB kwa kuendelea kuwa karibu na wateja wao kupitia kampeni mbalimbali zinazowapa motisha ya kutumia huduma za kidigitali.
Kwa upande wake, CRDB imeendelea kuwahamasisha Watanzania kutumia Tembo Card katika malipo ya kila siku ili kupata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo safari ya kwenda kushuhudia Kombe la Dunia pamoja na TV za kisasa za nchi 85.

Post a Comment

0 Comments