Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris awasili Tanzania

 





Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amewasili nchini Tanzania, tayari kwa kuanza ziara yake ya siku tatu nchini humo.

Ziara hii ya kiserikali inatokana na mwaliko wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati walipokutana jijini Washington mwaka 2022, ikitajwa pamoja na mambo mengine kuwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, sambamba na kuzungumzia maendeleo ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi.

Ziara yake imeanzia Ghana, Tanzania na kisha atamalizia Zambia.

Post a Comment

0 Comments