NaCONGO NA MHE. MWAKYEMBE WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUCHUKUA HATUA JUU YA TUHUMA ALIZOZITAJA KWA NGO's ZA USHOGA




Na: Teophil Mbunda, Dar es Salaam

 Baada ya siku chache Dkt Mwakyembe kuyataja baadhi ya Mashirika ya kiraia kujihisisha na Shughuli za kueneza maswala ya ndoa za Jinsia moja nchini (Ushoga) hii leo Baraza la Taifa la NGO's limetoa tamko lao juu ya hatua ambazo litazichukua juu ya tuhuma hizo.


Akiongea na Waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Lilian Badi amesema kuwa  wamefanyika kikao cha dharula cha Kamati tendaji kujadili, kuchanganua na kuweka maazimio ya utekelezaji kuhusiana na swala hilo.


Lilian ameeleza kuwa wao kama Baraza wamefanya mawasiliano na Mashirika yote ambayo yamehusishwa kwenye hutuma hizo, ikiwa ni maandalizi yake ya kufanya uchunguzi pamoja na mahojiano ya kina kwenye Baraza la maadili ya Kamati hiyo.


Pia Baraza ilo limeomba kukutana na Kamati ya Daktari Mwakyembe ili kupata taarifa yao na kuwaeleza namna watashughulilia swala hilo kama viongozi wa sekta ya NGO's.


Katika hatua hiyo Baraza la NGO's limewataka watanzania kuziona tuhuma alizotoa Dkt Mwakyembe ni tuhuma za swala mtambuka na sio NGO's pekeake ila hata wadau ambao hawakutajwa kwenye tuhuma hizo hivyo busara zitumike kwenye kushughulikia swala hilo.

Post a Comment

0 Comments