VICTOR MASANGU, PWANI
JAMII kwa kushirikiana na wazazi na walezi imeaswa kuweka mipango madhubuti ambayo itawasaidia watoto wa kike kukabiliana na changamoto mbali mbali zinawazowakabili ikiwemo suala la ukatili wa kijinsia ,ndoa pamoja na kupata mimba za utotoni ambazo zinapelekea kuwanyima haki zao za msingi hasa katika kupata elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkoa wa Pwani Bi.Mariam Ulega wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo yamefanyika kimkoa katika shule ya sekondari Bundikani iliiyopo Wilayani Kibaha ambayo yameandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Room to Read kwa kushirikiana na serikali .
Kwa upande wake Meneja miradi wa elimu kwa msichana na usawa wa Kijinsia Hadija Hassan amesems kwamba lengo la shirika lao la Room to Read ni kuweka mipango ya kuimarisha usawa wa Kijinsia katika kutoa elimu ya stadi za usomoji na kujenga tabia ya usomaji.
Naye Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani Sara Mlaki amebainisha serikali wanaunga mkono jitihada ambazo zinafanywa na Shirika hilo na kwamba watakuwa nao bega kwa bega katika kuona mradi huo unatekelezwa bila vikwazo vyovyote kwa lengo la kuwakomboa wanafunzi wa kike.
.jpg)
0 Comments