Waziri Wa Ujenzi Bashungwa ahitimisha ziara ya Miundombinu



Dar es Salaam:  Sheila  Ahmadi


Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi amesema

 itahakikisha Ujenzi wa barabara inayopita Kata nne ikiwemo Kisarawe 2 , Kimbiji, Pemba Mnazi Mwasonga yenye urefu wa  Km 47 itajengwa kwa kiwango cha lami ili kusaidia wananchi kuondokana na adha ya usafiri na kuifanya Kigamboni kuwa ya Uwekezaji.




Ameyasema leo Jijini Dar es salaam  Waziri wa Ujenzi Inocenti Bashungwa wakati wa Ziara yake ya Kikazi katika Wilaya ya Kigamboni  ambapo ametembelea barabara inayoanzia Kivukoni mpaka Kimbiji ambayo tayari imeshatengewa fedha na serikali kiasi cha Shilingi bilion 83.886 itaanza kujengwa kipande cha km 41 na km 7 zilizobakia Tanroad wanazifanyia usanifu .


"Wakati tunasubiria kusainia Mkataba na Mkandarasi nawaelekeza Tanroad kuwa barabara hii tuliyopita ina makorongo na matope sana hivyo ifanyieni marekebisho msisubirie mpaka Mkandarasi afike wananchi wanatakiwa angalau hata kama si kiwango cha lami lakini barabara zisiwe chafu sana" amesema Waziri


Waziri Bashungwa amesema Kigamboni ni eneo zuri sana kwani lina eneo maalumu ya Kuvutia  Uwekezaji Viwanda hivyo kipande hicho cha km 7ambacho hakijatengewa fedha Mhe Dkt Rais Rais Samia Suluhu Hassani tunakwenda kuzungumza naye ili nacho kijengwe kiwango cha lami kwani itasaidia kukua kwa Mji


Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu Mhandisi Dorothy Mtenga amesema barabara ya Kivukoni Kibada imeshajengwa Kiwango cha lami hivyo kipande kilichobakia kuunganishwa mkataba utakaposainiwa ikianza kukwangwua huku  itachukua  takribani ya miezi 20  mpaka kwenda kukamilika.



Aidha mhandisi huyo amesema kuazia kivukoni mpaka kibada barabara imejengwa katika kiwanja cha Lami hivyo mhandisi wa mkoa wa dar es salaam ndie ambae anasimamia wakati huku wanaendelea na mpango wa kujenga kiwango cha lami kwa hatua ambayo wamefikia kwa sasa kuazia kibada hadi mwasonga, tungi kwa kilomita 41.


Serikali  imeona umuhimu wa barabara hizo ziaze kujengwa kwa kiasi cha lami huku taratibu za manunuzi zinaendelea kufanyika hivyo kwa sasa wapo kwenye hatua ya mwisho katika manunuzi ya mwisho ya kusaini mikatba kwahiyo miradi ya miundombinu kigamboni inaenda kuanza kwani barabara hizo zinatumika kwa wakazi katika shughuli zao za kimaendeleo na baadhi ya viwanda vinahitaji miundombinu  iliyo sahihi ili kuchakata malighafi na kusambaza kwa wakati kwenda katika masoko "amesema Mhandisi  Mtenga"

Post a Comment

0 Comments