Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Heineken Beverage imeingia makubaliano na kampuni ya kitanzania Mabibo bia kwa ajili ya usambazaji wa bia ya Windhoek inayozatengenezwa nchini Namibia.
Hayo yamesemwa jijini Dar esalaam na Meneja kutoka Kampuni ya Heineken Obabiyi Fagade mara baada ya kuzungumza. Na wanahabari ambapo amesema kuwa lengo la kuingia ushirikiano huo ni mkakati mahususi wa kusaidia biashara za ndani na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania na kupata fursa za ukuaji katika ya kusini mwa Afrika.
"Ushirikiano huo na Mabibo bia ,wines na spirits ni kufungua ukurasa mpya kwa kuunganisha utaaalamu wetu wa Kimataifa Kama Heineken na ujuzi mkubwa walionao katika soko la ndani,tuna uhakika katika uwezo wetu wa kuwasilisha bidhaaa na huduma za kipekeee kwa watej wetu Tanzania";,amesema .
Aidha Heineken imedhamiria kutoa huduma za kipekeee kupitia vinywaji vyenje ubora wa hali ya juu ambavyo vinakizi ladha ya watumiaji.
Kwa. Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Bia Jerome Rugilamalila amesema mkataba huo wa kibiashara umekuja baada ya kampuni ya Mabibo na Namibia Breweries kukubalina kuvunja mkataba walioingia mwak 2008.



0 Comments