Na Mwandishi wetu
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Amos Lutakulemberwa Lwizamiaka mwenye. Umri wa miaka 54 mkazi wa Tegeta Wazo Kinondoni kwa tuhuma za kusambaza taarifa zisizo za kweli kwenye mitandao ya kijamii kuwa binti anayedaiwa taarifa zake kutoka mitandaoni hivi karibuni mwezi Agost 2024 kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa kubakwa na kulawitiwa amekutwa amefariki suala ambalo sio kweli
Akizungumza jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Murilo Amesema kuwa kupitia jeshi la polisi limeweza kumkamata Amos Lutakulemberwa ambae ametoa taarifa ya kufariki kwa binti ambaye amefanyiwa ukatili wa kinjisia ambapo sio jambo la kweli
" sisi kama jeshi tunatoa wito kwa wananchi katika kujiepusha na kutoa taarifa za uongo zenye malengo ya kuzusha taharuki katika jamii kwani kufanya hivyo ni makosa lakini litaendelea kuzingatia maoni ya watu ambayo hayakinzani na sheria za nchi," amesema SACP Muliro.
Aidha SACP murilo amesema. Kuwa hali ya usalama kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba katika Uwanja wa Benjamini Mkapa SACP Muliro ameeleza kuwa Jeshi hilo limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.
"Usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu. Jeshi linawakumbusha nimarufuku kwa mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo. Watu watakaojihusisha na vitendo vyakihalifu ndani au nje ya uwanjawatashughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria," amesisitiza SACP Muliro.

0 Comments