Foundation for civil society FCS Wametia saini ya makubaliano katika kulinda huduma za watumiaji wa mawasiliano Tanzania TCRA CCC

 

Na   Mwandishi  wetu

Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA CCC) zimetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitatu yenye lengo la kuimarisha juhudi za kulinda haki za watumiaji wa Huduma katika sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania.


Hayo  yamesemwa. Jijini  dar e salaam  na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS  Bw.Justice Rutenge ambapo  amesema kuwa    tunafahmu faida za  kuwalinda watumiaji dhidi ya mbinu za kibiashara zisizo za haki katika soko.


"Makubaliano  hayo  yanaenda kuhakikisha haki na uwajibikaji katika kutoa Huduma kwa watumiaji na kiwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa na Huduma za kulinda haki za watumiaji (Consumer Protection)unachangia maendeleo ya masoko na ukuaji wa biashara" amesema Rutenge.


Hata hivyo  aliongeza kuwa Biashara zinazoheshimu sera za kulinda watumiaji na kuwapa wateja wao kipaumbele hujijengea hadhi na kuziweka katika nafasi nzuri kiushindani,hii huzihakikishia biashara hizo uwepo wa wateja wa uhakika na kuweka meingi mzuri wa ukuaji.


  kwenye   soko la sasa lenye mabadiliko ya haraka,uadilifu katika biashara unategemea kwa kiasi kikubwa kulinda haki za watumiaji dhidi ya mbinu zisizo za haki na udanganyifu katika biashara.


Bw.Rutenge ameongeza kuwa  Wafanyabiashara Wana nafasi muhimu katika kuhakikisha uwazi na usahihi katika shughuli zao,hivyo FCS na TCRA CCC zimeunganisha nguvu katika kubuni na kutekeleza mradi unaolenga kulinda haki za watumiaji wa bidhaa na Huduma za Mawasiliano nchini Tanzania.


Naye   Katibu Mtendaji wa TCRA CCC ,Bi.Mary Shao Msuya amesema kwamba Baraza Hilo limeanzishwa kwa lengo la Kuhakikisha maslahi ya watumiaji wa Huduma za Mawasiliano za TEHAMa,Huduma za Utangazaji,Huduma za Posta,na Virus Hi na Vipeto.


Aidha  amesema  kuwa huduma za Mawasiliano nchini zinaongezeka kitokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia kwa mujibu wa takwimu za TCRA ,kufikia June,2024 kuna kadi za simu milioni 76.6,watumiaji wa internet milioni 39.3,akaunti za pesa mtandao milioni 55.7, ambapo idadi hiyo itaendelea kuongezeka na Huduma mpya zitaongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kidijitali.


"Kupitia   teknolojia  hii ni muhimu hasa wakati nchi yetu imejukita kwenye uchumi wa kidigitali ,Mawasiliano yanaweza kufikisha taarifa kwa wakati ,uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Biashara,uzalishaji ,elimu,afya na upatikanaji wa Huduma jumuishi za kifedha.

Post a Comment

0 Comments