HESLB , KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA NIDA, RITA, CREDITINFO WAMEBADILISHANA HATI ZA MAKUBALIANO KATIKA KUWASAKA WADAIWA SUGU WA MIKOPO.

 


Na  Sheila  Ahmadi

Bodi ya mikopo ya wanafunzi  wa elimu ya juu (HESLB). Imebadilishana hati 
Za makubaliano na Taasisi Kadhaa za kimkakati ambazo zinaenda kutekeleza kwenye utoaji wa taarifa katika kuwasaka wadaiwa sugu wa mikopo ambao walipewa kipindi wako vyuoni na kushindwa  kurejesha  kwa wakati.




Hayo  yamesemwa  jijini  Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji  wa bodi ya mikopo  ya elimu ya juu (HESLB) Bill Kiwia  amesema kuwa  lengo  la kubadilishana hati za makubaliano na taasisi hizi  ni kuweza kuongeza mbinu ya kuwapata wadaiwa sugu wa mikopo hiyo hususani wale walioko kwenye sekta binafsi na isiyo rasmi kwa matumizi ya mifumo ya tehama.



  "Bodi ya mikopo  inatoa   rai  kwa wanufaika wa mikopo Hiyo  ambayo walipewa ili waweze kurejesha mikopo kwa wakati ili wengine waweze  kwenda vyuoni  kuendelea na masomo huku Taasisi Ya Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, wakala wa usajili ,ufilisi na udhamini RITA,taasisi za uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye taasisi za fedha CREDITINFO zikiwa tayari kwa majukumu ya kuwasaka wadaiwa hao.



Aidha  MKurugenzi Kiwia ameongeza kuwa katika ukusanyaji wa mikopo hiyo tunawakaribisha wadau hawa katika kwenda kufikisha ujumbe huu kwa kutumia Mifumo ya tehama.



Kwa  upande wake Kaimu Mkurugenzi mkuu kutoka 
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa nida Deusdedit buberwa amesema kuwa tutashirikiana vyema katika kutekeleza makubaliano  ya serikali huku taasisi za kiserikali zikiweza kuunganisha mifumo ya  tehama  katika kutoa huduma kwa wananchi.




Naye  Mtendaji  mkuu  kutoka RITA. Frank kanyusi  amesema kuwa tuna jukumu la kutoa vyeti vya uzazi na Vifo  katika kuweza kukamilisha suala hilo la wadaiwa hivyo sisi kama Rita tumeweza kujiunga na mfumo wa kieletronik ili kumwezesha kupata Cheti ambapo bodi ya mikopo watahitaji kuona vyeti vya muombaji wa mkopo ili kuhakikisha kuwa ana visibitisho vyote .


Vilevile mtendaji mkuu kutoka CREDITINFO  Edwin  Urasa  ameongeza kuwa  wanufaika wa mikopo hiyo ya elimu ya juu  waanze kujitokeza na kurejesha mikopo kwa wakati sahihi ili taasisi za fedha ziweze kukopesha wanavyuo wengine ambao wanatarajia kwenda vyuoni hivi karibuni.






Post a Comment

0 Comments