GSM foundation imeahidi kuendeleza ushirikiano na hospitali ya Ocean road kwa kutoa vifaa tiba na huduma za kiafya kwa wagonjwa wa saratani.
Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Taasisi Faith Gugu wakati wa maadhimisho siku ya Saratani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Taasisi yetu imejikita zaidi katika kuisaidia jamii hivyo mara nyingi huwa tunaisapoti hospitali hii kwa kutoa huduma za kiafya kwa kutoa vifaa tiba na misaada inayoendana na huduma za afya,” alisema
Vile vile aliongezea kuwa kwa mwaka taasisi hiyo imetoa T-shirt kwa ajali ya matembezi yaliyofanyika kwa ajili ya maadhimisho hayo.Pamoja na kutoa katoni 100 za maji.

0 Comments