RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika maombi ya kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi mkuu wa Raisi,
Wabunge, Madiwani unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Ibada hiyo itafanyika Febuari 22 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.Hayo yalisemwa na viongozi wa Dini kutoka umoja wa ma Kanisa ya kiroho.
Askofu Paul Bendera wa Kanisa la Ufunuo alisema kuwa ibada hiyo itafanyika siku nzima lengo la kufanya ibada hiyo ni Mara baada ya kuguswa na maendeleo yaliyofanywa na Raisi Samia tangu alivyoingia madarakani.
“Tanzania ni nchi miongoni kwa nchi yenye amani hivyo sisi kama viongozi wa Dini, kuelekea uchaguzi mkuu inatupasa tuliombee taifa liendee kuwa na amani kama ilivyo awali,”alisema
Amesisitiza Watanzania kujitokeza ili kuliombea taifa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Naye Askofu Hellen Tusiime kutoka Divine Hope International Church alibanisha kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kusali ili mambo yaweze kuwa rahisi.
Kwa upande wake Askofu Amoke Nkonoki kutoka Kanisa la Heart of Worship alizungumza amewakaribisha watu wa Dini zote na makabila yote kuhudhuria ibada hiyo.
Askofu Allen Siso kutoka Tanzania Methodist Church alisema kuwa anafurahishwa kumuona Raisi wa Tanzania ni mwanamke na kufanya maendeleo na majukumu yake kama inavyotakiwa.
“Wananchi wote yatupasa kumuombea Raisi wetu kwa kazi anayoifanya na atakayoiendeleza,”alisema


0 Comments