Na Nancy Mawole
BONDIA Amir Matumla anatarajia kupambana na bondia kutoka Namibia Paulus Amavila katika pambano lisilokuwa la ubingwa lenye raundi 8 uzito wa ‘super weight’ litakalofanyika Februari 28 mwaka huu.
Akitangaza mapambano ya Knockout ya Mama Dar es Salaam Leo Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba amesema pambano litafanyika jijini Dar es Salam.
Amesema anatarajia bondia Amir ambaye ni mtoto wa bondia wa zamani Rashid Matumla atafanya vizuri kwani ana hamu ya kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi.
"Tumezungumza na bondia huyu alihimiza tumtafutie pambano la kimataifa kwa hiyo litakuwa pambano lake la kwanza kwake la kimataifa,"amesema.
Zayumba amesema lengo la pambano hilo ni kuendelea kumsapoti Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa ni mwanamichezo namba moja hivyo, watatumia pambano hilo kuendelea kutangaza mazuri aliyofanya.
Kwa upande wake Amir amesema:" Nashukuru sana Mafia kwa kunipokea, naahidi Watanzania nitaendeleza kwa ukubwa zaidi, sasa hivi naendelea na mazoezi, watu waje kwa wingi kuangalia na kufurahia pambano hilo.”
Naye Balozi wa Mafia Boxing Promotion ambaye pia ni Mwanamziki wa Bongo Fleva Nurdin Bilal 'Shetta' amewaasa mabondia hawa kutumia nafasi waliyopata kujitangaza kimataifa pamoja na kujikwamua kiuchumi.

0 Comments