WAFANYABIASHARA WA TANDIKA WAKUTANA KUWASILISHA CHANGAMOTO ZAO.




Na Nancy Mawole 


JUMUIYA ya wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam imeendeleza ziara yake ya kuwatemmbelea wafanyabiashara wa eneo la Tandika lengo uhamasishaji wa kulipa stahiki na kwa wingi.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.


Akizungumza Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzindua product mpya ya ‘Tunaweza’ pamoja uzinduzi wa mabalozi katika eneo hilo.


“Sisi kama jumuiya tutahakikisha wafanyabiashara wote wanalipa kodi kulingana na biashara zao bila uonevu wote pamoja na kumiliki TIN namba na lesseni,” alisema 


Naye Riziki Ngaga Katibu wa Wafanyabiashara katika Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa wiki ijayo wanatarajia kutembelea eneo la Ilala .


Amesema lengo la ziara hii ni kutatua changamoto zinazowakumba wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali.


Miriam Malongoli ambaye ni mfanyabiashara amefurahishwa na kikao hicho ambapo wametoa malalamiko juu ya kodi, na tuzo nyingine na ana amini malalamiko hayo yatafanyiwa kazi.

Post a Comment

0 Comments