Na Francisco Peter, Dar es Salaam
Mara baada ya kuapishwa rasmi, ameahidi kutatua kero mbalimbali zinazowakumba Wananchi wa Buyuni ikiwemo miundombinu ya Barabaraa, Elimu, Afya Maji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii.
Diwani wa kata ya Buyuni Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe.Jesca Mahamoud Msolla amesema kuwa kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi atahakikisha anashirikiana Vyema na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Nurdin Bilal Juma(Sheta) na Naibu wake Jonh Ryoba Mrema pamoja na watendaji wa Halmashauri ya jiji hilo katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa kata ya Buyuni.
"Tunahakika tumemchagua Mstahiki Meya(Nurdin Bilal Juma) na naibu wake(Jonh Ryoba Mrema),pia sisi madiwani tumeapishwa rasmi ikiwa ni hatua ya kuanza kushiriki katika Baraza la Madiwani kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo"amesema Mh.Jesca kwa bashasha kubwa.
Vile vile ameaongeza kuwa amejipanga vizuri kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali za kata nakutamani kata ya Buyuni iwe na maendeleo makubwa,na hivyo yeye kama diwani atahakikisha malengo hayo yanafanikiwa.


0 Comments