MCHANGE ATAJA WANAHARAKATI WA NJE KUCHOCHEA VURUGU, AITAKA KENYA NA MAREKANI KUTOA USHIRIKIANO

 



Habari


Mchange amesema leo, tarehe 17 Desemba 2025, kuwa mbegu za vurugu zilizojitokeza tarehe 29 Oktoba pamoja na zile zinazoendelea kuhamasishwa kwa sasa, zinatokana na baadhi ya wanaharakati waishio nje ya Tanzania, hususan katika nchi za Kenya na Marekani.


Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA), Bw. Habibu Mchange, alisema kuwa watu wanaochochea vurugu, mauaji na kutokuheshimu mamlaka ya nchi hawapo ndani ya Tanzania, bali wapo nje ya nchi, huku madhara yote ya vurugu hizo yakiwakumba Watanzania waliopo nchini.


> “Mbegu za vurugu za tarehe 29 Oktoba na hizi wanazoendelea kuhamasishana zinatokana na baadhi ya wanaharakati waishio nje ya Tanzania ambao wapo Kenya na Marekani,” alisema Mchange.




Aliongeza kuwa MECIRA haitaendelea kukaa kimya wakati amani ya taifa inavurugwa na watu walioko nje ya mipaka ya nchi.


> “Wanaochochea vurugu, mauaji na kutokuheshimika kwa mamlaka za nchi wapo huko kwenye hayo mataifa yao. Sisi kama MECIRA hatutakaa kimya na tutaendelea kulisema hili kwa sababu kinachofanyika ni kuvuruga amani ya nchi yetu,” alisema.




Mchange alisema kuwa wahusika hao wanafahamika wanapoishi katika nchi hizo na tayari maombi yamewasilishwa kwa balozi husika ili wahusika warejeshwe nchini kujibu tuhuma zinazowakabili.


> “Hao wanaochochea wanafahamika mahali wanapoishi katika hizo nchi. Tumeziomba balozi ziturudishie hao watu. Hili jambo si la serikali peke yake, bali Watanzania kwa pamoja lazima tuungane kuipigania Tanzania. Hawa watu lazima warejeshwe nchini kujibu kesi hizi za kusababisha vurugu,” alisema.




Akifananisha matukio hayo na rushwa, Mchange alisema kuwa aliyechochea na aliyetekeleza wote wanabeba dhamana ya madhara yaliyotokea.


> “Hii ni kama rushwa, aliyetoa na aliyepokea. Wao ni sehemu ya matokeo ya vifo vilivyotokea kutokana na vurugu hizo walizozipanga. Hakuna haki bila wajibu,” alisisitiza.




Katika hatua nyingine, Mchange alimtaja mwanaharakati Maria Sarungi kuwa amekimbilia Nairobi nchini Kenya na baadaye kuelekea nchi za Skandinavia, akisisitiza kuwa jitihada za kisheria zinaendelea.


> “Tunafahamu Maria Sarungi amekimbia Nairobi huko Kenya na kukimbilia Skandinavia. Tutamfuata na tutaenda kuwashtaki mpaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Lazima hawa watu wanaochochea wakamatwe,” alisema.




Aidha, alisema kuwa waathirika wa vurugu zote wapo ndani ya Tanzania, huku wachochezi wakiwa nje ya nchi, jambo alilolitaja kuwa halikubaliki.


> “Watu wote wanaoshawishi vurugu hawapo Tanzania, walioumizwa na kuathirika na madhara ya vurugu wapo Tanzania,” alisema.




Mchange aliwataka Watanzania kushirikiana na kupaza sauti kwa jumuiya ya kimataifa, akisisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru lenye uwezo wa kujiendesha.


> “Watanzania tushirikiane na tupaze sauti kuiambia dunia kwamba tunafahamu kinachoendelea. Tunataka Marekani iheshimu uhuru na mamlaka ya Tanzania. Tunaweza kujiendesha,” alisema.




Alimtaja pia Mangi Kimambi kuwa ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kuchochea vurugu akiwa nje ya nchi, akidai kuwa amejificha nchini Marekani.


> “Tunafahamu yupo muarifu ambaye ni Mangi Kimambi amejificha Marekani. Tunatambua wanapambana na waharifu na muarifu mmoja wapo ni Mangi yupo kwenye ardhi yao. Wamrudishe kwa sababu amekuwa sehemu ya kuchochea vurugu nchini,” alisema.




Mchange alidai kuwa Mangi Kimambi amekiri kuwa hatua ya kampuni ya Meta kuzuia akaunti zake ilisaidia kukwamisha vurugu zilizopangwa kufanyika Desemba 9, huku akiwashukuru raia wa Kenya kwa msaada anaodai kupewa.


> “Mangi amekiri kwamba kitendo cha Meta kuzuia akaunti zake kimekwamisha vurugu za Desemba 9. Pia amewashukuru Wakenya na kusema waendelee kuwasaidia. Tunajua wanaowatunza hao akina Hilda Newton wapo Kenya na wanahusika na machafuko,” alisema.




Alitoa wito kwa Serikali za Kenya na Marekani kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote wanaotuhumiwa kuchochea vurugu.


> “Tunaitaka Kenya na Marekani kutoa ushirikiano wao katika kuwakamata

Post a Comment

0 Comments