Dar es Salaam:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Faida Fund kwa kuendelea kuonyesha mafanikio makubwa, ikiwemo ongezeko la uwekezaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 18 tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza leo, tarehe 17 Januari 2025, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Mwaka wa Faida Fund, Waziri Kikwete alisema anajivunia na kufurahishwa na maendeleo makubwa yanayopatikana ndani ya mfuko huo unaolenga kuwawezesha watumishi wa umma kushiriki katika uwekezaji wa makazi na miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Binafsi naona furaha na fahari kubwa kushuhudia maendeleo makubwa ya Faida Fund, mfuko unaoendeshwa kwa ufanisi mkubwa chini ya Watumishi Housing Investment,” alisema Waziri Kikwete.
Alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi mzuri wa menejimenti, matumizi ya mikakati madhubuti ya uwekezaji, pamoja na kuimarika kwa imani ya wawekezaji, hali iliyopelekea ongezeko kubwa la mtaji ndani ya mfuko huo.
Katika hatua nyingine, Waziri Kikwete aliitaka menejimenti ya Faida Fund kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kubuni mbinu bora zaidi za kuwafikia wawekezaji wengi, hususan watumishi wa umma waliopo ndani na nje ya mifumo rasmi ya ajira.
Aidha, alisema Serikali inatarajia kukutana na Faida Fund mwezi Juni, ambapo itazindua rasmi Mfuko wa Uwekezaji wa Watumishi wa Umma kupitia portal maalum, hatua ambayo tayari imeanza kuzaa matunda baada ya watumishi zaidi ya 1,200 kujiunga na kuwekeza.
“Wawekezaji wenye sifa kama zenu ni wengi sana; ninawahimiza mtumie vigezo na mifumo ya Serikali kuwafikia na kuwashirikisha watumishi wengi zaidi,” alisisitiza Waziri Kikwete.
Pamoja na pongezi hizo, Waziri Kikwete alitoa wito kwa Faida Fund kuendelea kuzingatia misingi ya utawala bora, uwazi na ulinzi wa mitaji ya wawekezaji, akihakikishia kuwa Serikali itaendelea kuusimamia na kuuthamini mfuko huo.
“Serikali itaendelea kusimamia Faida Fund na kuhakikisha usalama wa fedha za wawekezaji,” aliongeza.
Waziri Ridhiwani Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mfuko wa Tatu wa Wawekezaji wa Faida Fund, tukio lililothibitisha dhamira ya Serikali ya kuimarisha mifumo ya uwekezaji kwa watumishi

0 Comments