Dar es Salaam – Mstahiki Meya wa Temeke, Uzairu Athumani, ameshiriki kikamilifu katika mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika wilayani humo, akishirikiana na wananchi katika kuupokea na kuukimbiza mwenge huo.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa mbio hizo, Meya Uzairu alimshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli hiyo muhimu, akieleza kuwa wananchi wa Temeke wameonesha mshikamano mkubwa katika kushiriki tukio hilo la kitaifa.
“Namshukuru Mungu, Temeke tumemaliza kuukimbiza Mwenge wa Uhuru tukishirikiana na wananchi wetu,” amesema.
Ameongeza kuwa katika mbio hizo, Mwenge wa Uhuru umepita katika maeneo mbalimbali kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo, hatua inayolenga kuhamasisha uwajibikaji na kasi ya maendeleo katika jamii.
Aidha, amepongeza ushirikiano wa wananchi na viongozi mbalimbali uliofanikisha zoezi hilo, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kulinda na kuendeleza miradi iliyozinduliwa kwa manufaa ya wakazi wa Temeke na taifa kwa ujumla.
Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo, umoja na uzalendo miongoni mwa Watanzania



0 Comments