TUCHUKUE TAHADHARI LEO, TUOKOE MAISHA NA MALI KESHO MPOGOLO



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari mapema ili kuzuia madhara ya majanga mbalimbali yanayoweza kugharimu maisha na mali.

Akizungumza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa sherehe na maonesho kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazimamoto Duniani, Mhe. Mpogolo alisema maadhimisho hayo yanalenga kutambua mchango mkubwa wa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kukabiliana na majanga.

Alibainisha kuwa jeshi hilo limekuwa mstari wa mbele katika kukinga na kuokoa maisha ya wananchi wakati wa matukio ya moto, matetemeko ya ardhi, mafuriko, maporomoko ya ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine ya dharura.

Maonesho hayo yanaendelea katika viwanja hivyo hadi Mei 4, 2026, ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania litaungana na wazimamoto duniani kote kuadhimisha siku hiyo inayofanyika kila mwaka.













Katika maadhimisho ya mwaka huu, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila.

Kauli mbiu ya mwaka 2026 inasema: “Tuchukue tahadhari leo, tuokoe maisha na mali kesho.”

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho hayo ili kujifunza mbinu za kujikinga na majanga pamoja na kuimarisha ushirikiano na vyombo vya uokoaji.

Post a Comment

0 Comments