MEYA KIGAMBONI NA TARURA MKOA WA DAR KUCHOCHEA UJENZI WA MIHUNDOMBINU YA BARABARA



Meya Kigamboni apania Bega kwa Bega na TARURA  Mkoa Dar,  Kuchochea Ujenzi Mihundombinu ya B

Na Francisco Peter, Dar es Salaam 

Mstahiki Meya wa  Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Amini Nzuri Sambo amesema kuwa  baadhi ya kata  zinaupungufu wa mihundombinu ya barabara.

Amezitaja baadhi ya kata hizo, kuwa ni Kibada , Kimbiji Somangilo, pamoja na kata ya Pemba Mnazi .

Akizungumzia juu ya mihundo minu hiyo sikuchache zilizopita Jijini Dar es Salaam  Sambo amesema  kuwa yeye k sasa ni Meya maana yake anaingia bodi ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini - (TARURA),Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo hali hiyo  ni moja ya kichocheo cha kuleta fursa.

"Tahakikisha napigania kwa nguvu zote  napigania juu ya maendeleo ya wananchi katika kuondoa kero zinazo wakabiri wananchi  huku nikihakikusha wanapata Miundombinu bora ya bara bara,"amesema meya Sambo.

Sambo amewaomba kwa wakati huu wananchi kuanza kushirikiana na vipngozi na kwamba popote kwenye mapungufu wananchi kusema hali itakayo harakisha kupatikana kwa maendeleo kwa haraka.

Aidha meya huyo amewaelekeza wananchi kuwatumia vema viongozi , ili wawe wawakilishi kwa kuwa yapo mambo yanayo fanyika wanakosa uthibiti.

Vile vile kiongozi huyo ameelezea kuhusu daraja la kigamboni ambapo amesema atachukua jukumu la kuonana na wahusika kupata maelekezo  sahihi kujua makubaliano yaliyopo.

"Takwenda kuona  muongozo  kati ya makubaliano yaliyopo,  kati ya serikali na NSSF basi yakiwa yapo kimkataba  litakuwa ni jambo la kufikiria kwamba mkataba huo unasema nini na inasimama vipi," amesema Sambo.

Kati hatua hiyo ameelezea mara baada ya juhudi hizo kufanyika ndipo atakapo kuja kuelimishana na wananchi.

Wakati huo huo meya huyo ameelezea kuwa wakati daraja hilo linajengwa wananchi walikuwa na uitaji hata kwa bei kubwa sasa tukaujue kama hautatuliki.

Post a Comment

0 Comments