NA MWANDISHI WETU,DODOMA
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimeadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukata keki na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira na6 kuhakikisha Jiji la Dodoma linaendelea kuwa la kijani.
Akizungumza mapema leo, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga, amesema kuwa maadhimisho hayo yamelenga kuenzi mchango mkubwa wa Rais Samia katika kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira nchini, hususan katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema Dkt. Samia ni mwasisi wa harakati za upandaji miti nchini, akieleza kuwa akiwa Makamu wa Rais alizindua zoezi la upandaji miti katika eneo la Makutupora mkoani Dodoma, jambo lililoweka msingi wa
Mbanga ameongeza kuwa CCM Mkoa wa Dodoma imeona ni jambo la muhimu na la heshima kubwa kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti, kama njia ya kuendeleza maono na mwelekeo wa Raisb Samia katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.


0 Comments