NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Uongozi wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini umewahimiza wanawake kuhakikisha kwamba wanajiunga kwa pamoja katika kujiunga na vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ikiwemo kutumia fursa za kuchukua mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kiuchumi na kuondokakana na wimbi la umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja wakati wa ziara maalumu yenye lengo la kuweza kuwashukuru wanawake kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kupelekea chama cha mapinduzi (CCM)7 kuweza kushinda kwa kishindo katika viti vitatu vya Udiwani, Ubunge pamoja na nafasi ya Urais.
Mwenyekiti huyo ameweza kufanya ziara hiyo maaalumu katika kata mbili za Maili moja na Kata ya Tangini ambapo ameongozana na baaadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa lengo la kuweza kuzungumza na wanawake hao kusikiliza baadhi ya chanagmoto zao pamoja na kuwashukuru kwa kukipigia kura nyingi za kishindo chama cha mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwapata viongozi wa nafasi mbali mbali.
"Tumeanza ziara yetu tangu tarehe 10 mwezi huu na lengo letu kubwa ni kutembelea katiika kata zote 14 kwa ajili ya kukutana na wanawake ikiwa ni kutoa shukrani za dhati nikiwa pamoja na katibu wangu wa UWT ambapo tumeongozana kwa pamoja na baadhi ya wajumbe wwa kamati ya utekelezaji ambapo kwa leo tumefanya ziara katika kata ya Mail moja na pamoja na Tangini.
Pia Mwenyekiti huyo amebainisha kwmaba lengo lingine la ziara hiyo ya kuweza kuimarisha jumuiya hiyo kuanzia ngazi za matawi na kuwataka viongozi mbali mbali wa matawi kuhhakikisha wanavunja makundi na kuungana kwa pamoja kwani uchaguzi mkuu umeshamalizika hivyo kitu kikubwa ni kuwa na umoja na mshikamano.
Kadhalika Mwenyekiti huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita kwa kuweza kutekeleza ilani ya cchama kwa vitendo ikiwemo kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, eilimu, maji, nishati ya umeme pamoja na huduma za kijamii.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Cesilia Ndalu amebainisha kwamba ziara hiyo pia imelenga kuanzisha vikundi vya uchumi ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kukubwa kupambana na wimbii la umasikini.
Diwani wa kata ya Mail moja Ramadhani Lutambi ameahidi kuzishughulikia changamoto mbali mbali walizonazo wanwawake ikiwemo suala la kuweza kuwasimamia kujiungha katika vikundi mbali mbali vya ujasiriamali pamoja na kuwapambania kuweza kupata fursa za mikopo ambayo itawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.
Ziara ya jumuiya ya wanawake Wilaya ya Kibaha mjini ambayo ilianza rasmi tangu Machi kumi mwaka huu imeweza kuleta mafanikio makubwa naakupokelewa na wanawake kutoka kata mbali mbali amnbao wameweza kutoa pongezi zao za dhati kwa ziara hiyo ya uongozi wa UWT ambayo imeweza kuleta matumaini makubwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

0 Comments