AML FINANCE LIMITED YAZINDUA KAMPENI YA “KAMATA MKWANJA” DAR ES SALAAM








Dar es Salaam, Aprili 13, 2026 – Kampuni ya huduma za kifedha, AML Finance Limited, imezindua rasmi kampeni yake mpya ya “Kamata Mkwanja” yenye lengo la kuwawezesha Watanzania kupata mikopo na huduma mbalimbali za kifedha kwa urahisi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Aniel Wisye Mwakatobe, alisema kampeni hiyo inalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kutoa fursa za kifedha kwa sekta mbalimbali za uzalishaji.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, huduma zinazotolewa ni pamoja na mikopo kwa shule, wakandarasi pamoja na wadau wa sekta zote za uzalishaji uchumi, hatua inayolenga kukuza biashara na maendeleo ya wananchi.

Aidha, kampuni hiyo inatoa huduma za mikopo ya magari (car loans) pamoja na huduma za bima, ikiwa ni sehemu ya suluhisho jumuishi kwa wateja wake.

Katika muundo wa uongozi wa kampuni hiyo, Carolyn Lymo ni Mkuu wa Idara ya Mikopo, huku Mpoki Richard akiwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara, na Lydia Machangu akihudumu kama Mkuu wa Fedha.

Pia, kampuni hiyo inaongozwa kwa upande wa uendeshaji na Afisa Mkuu wa Uendeshaji (COO), huku ikijikita katika kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake.

Mbali na huduma za kifedha, AML Finance Limited pia inamiliki jengo la AM Tower, linalotoa nafasi kwa wafanyabiashara na kampuni mbalimbali wanaohitaji maeneo ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi.

Uzinduzi wa kampeni hiyo unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya sekta binafsi, huku ukiwapa Watanzania wengi zaidi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments